Mtunzi: Lasima
Nassoro Samson amekimbia na mzigo
wa Bwana Kanjubai? je samson amekimbilia wapi? je nini kitatokea akigundulika
alipo?...endelea....
Wakati Teresia akiendelea kuwaza kuhusu mustakabali wa
maisha yake, simu ikaita, akakurupuka toka
pale alipokaa kwenda kuchukua simu akifikiri ni Samson anayempigia,
alipoangalia jina la mpigaji akaona ni rafiki yake aitwae Jamila, "vipi shost,
mbona leo haujafungua kibanda chako?", Jamila alimuuliza Teresia.
Teresia hakufurahi alipoona kuwa mpigaji hakuwa Samson
hivo hakupenda kuwa na mazungumzo marefu na Jamila, akamjibu,
"sijisikii vizuri leo, nahisi nitakuwa na
malaria".
"hata mie nilifikiri tu kuwa utakuwa unaumwa maana si kawaida yako
kuacha kufungua, pole mwaya, nitakupigia kesho kuangalia kuwa unaendeleaje, ila
kama hujaenda hospitali, kesho asubuhi na mapema uende ukachekiwe, sawa
shosti?".
"nashukuru, nitafanya hivo, usiku mwema",
alipomaliza kumuaga Jamila, Teresia hakusubiri jibu
maana anamfahamu vema Jamila kuwa
kama hata kata simu, Jamila ataanzisha
stori za umbea alizo sikia mchana
kutwa.Teresia alikuwa akitazama Tv lakini akili yake na mawazo yote
yalikua kwa Samson, alikumbuka jinsi walivoanza urafiki wao baada ya Samson kuwa
mteja wake mzuri, karibia kila siku ambazo hakusafiri, alikuwa akienda kula
chakula katika kibanda cha Teresia, siku hiyo Samson akamuambia
Teresia,
"leo usiku naomba nikutoe"
Teresia akajifanya hajamuelewa, "unitoe nini?,na kwanza sijakuambia kuwa nina
kitu nataka nitolewe".
Samson
akatabasam kisha akasimama pale alipokuwa amekaa na kwenda alipokaa
Teresia,akashika pua ya Teresia na kuitingisha tingisha,akamuambia,
"you are a naught girl".
"wengine hatujui
kidhungu,usije ukawa unanitukana".
"hahaha,sijakutukana,nimesema kuwa
umeumbwa ukaumbika".
Samson akakaa karibu na alipokuwa amekaa Teresia.
Teresia alipoambiwa kuwa ameumbika,akahisi soni ikimuingia machoni, akashindwa
kumuangalia Samson machoni, akaamua kutoka pale na kwenda kukusanya vyombo
vilivyotumika. Kabla hajafikia vile vyombo,Samson akamshika mkono na
kumzuia
asiondoke pale alipo,akamuambia,
"mbona wataka kunitoroka kabla hatujafikia
muafaka?"
Kitendo cha Samson kumshika mkono,Teresia alihisi kama ameshika
waya wa umeme,mwili wote ulimsisimka, akakosa jibu la kumuambia Samson. Samson
alipoona Teresia hasemi lolote, akamkalisha mbele yake nakumuangalia
machoni,"bibie,mbona umekuwa mpole ghafla,nimesema neno lolote lililo kukerehesha?". Teresia
akatingisha kichwa kuonyesha ishara ya kuwa hakuna, bila kusema neno.
"kwani
umekuwa bubu?, Teresia chiriku ameenda wapi?". Baada ya Samson kumuachia,Teresia
alirudia hali yake ya kawaida,akamuambia Samson,
"nilikuwa nakupima kama wewe ni jasiri au
la".
Samson akasimama,
"wanipima kuwa mi ni jasiri kwa kigezo gani?, kwanza
hakuna kitu nilichoona hapa cha kunipima".
"nilipokaa kimya,nilikuwa nakupima
kama utakasirika na kuamua kuondoka ama utaonyesha kujali".
Samson
akacheka,
"kama hilo ndio lilikuwa kusudio lako,umenipata maana
nilijihisi mkosaji, sasa tuachane na hayo,je umekubali twende club?".
"twende
club kufanya nini?,mie sinywi pombe".
"acha ushamba,sio club za pombe,ni club
za magoma kitakita,kwani hupendi muziki?".
"napenda ila sijawahi kwenda disco
toka nizaliwe".
"basi ngoja iwe mara ya kwanza,twende ukasikie muziki kama
ule usemao",
Samson akarekebisha koo kisha akaanza
kuimba,
"nachungulia dirishani ooh,naona ni mvua yanyesha eeh,
hakuna kilichobakia ooh, ila ni uchungu na huzuni eeh,mpenzi nauliza utarudi
lini eeh, uje unitoe upwekwe na huzuni eeh,s heri rudi rudi mpenzi wa roho,
sheri rudi mie nakufa kwa pendo, elewa dada nakupenda kwa uzuri wako, nakuomba
utoroke eeh maana nakufa kwa upwekwe,njoo dada tuishi kwa upendo, ni wewe tu
uliyeuteka moyo wangu,nakupenda kwa dhati", wakati wote huo Samson alipokuwa
anaimba,alikuwa amefunga macho, Teresia akamuangalia jinsi alivojengeka
kimaumbile, akahisi kumpenda Samson, alitamani awe wake peke ake. Samson
alipofungua macho, akaona jinsi Teresia alivokuwa anamuangalia kwa macho ya
mahaba, moyo wake ukamuenda mbio, akatamani amkumbatie na kum'busu lakini aliona
kuwa anaweza kuharibu kila kitu, akajiambia mwenyewe kichwani mwake,'hawa watoto
wa kutoka kijijini, hawatakiwi papara,
mwendo wa kinyonga tu hadi tutafika', akatabasam. Teresia akamuuliza,"watabasam
nini?".
Samsoni akamjibu,
"unajua kama ukiamka asubuhi na kitu cha kwanza
kukiona chapendeza machoni,shurti
utabasam".
"lakini sasa hivi si asubuhi, ni usiku".
"nafahamu hivo,wakati
naimba nilipofungua macho, macho yangu yakakutana
na ua waridi lipendezalo kuliangalia wakati wote bila kuchoka".
"eeeh!
makubwa,haya hilo ua liko wapi?, maana mie silioni,isije ikawa upo ulimwenguni mwingine mie sijui".
"nimimi
peke yangu nilionae,sasa club tunaenda?".
"sawa, ila sitaki nichelewe kurudi
maana wajua shughuli zangu,saa kumi na
moja alfajiri natakiwa niwe nimeshaamka".
"usijali, tukiruka ngoma mbili
tatu, tutarudi".
"sawa, ila sikujua kuwa we ni muimbaji".
"kwani
nimekuambia kuwa mimi ni muimbaji?".
"hujaniambia bali nimekuona ulivyokuwa
unaimba huo wimbo kwa hisia kama vile wamuimbia mpenzi wako".
Samson akacheka
kisha akamuambia ,
"sasa katika waimbaji na mie nitasema nimo?, si watu
watanikimbia na kuniacha peke yangu wakisikia hili lisauti langu linalo fanana
nala chura".
"hamna,umeimba vizuri kweli, ningeweza ningekutunza".
"kama
hivo ndivo,basi kesho msosi utanipa bure,t ena si kidogo kama huu unaonipimia?,
msosi wa kushiba na kikombe cha chai au kahawa".
"hehehee, uliona wapi mbuzi
na kuku wakishirikishwa kupanga tarehe ya krisimasi?".
"una maana
gani?".
"maana yangu nikuwa,mtu hajichagulii zawadi, we subiria na uwe mpole
kama kondoo apelekwae mnadani".
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa mapenzi kati ya
Samson na Teresia,ambapo baadae waliamua kuishi pamoja kama mke na mume. Teresia
aliendelea kukumbuka jinsi alivyokuwa akimuuliza mara kwa mara Samson kuwa ni aina gani ya kazi aliyokuwa
akifanya,mara zote jibu lilikuwa,
"vuta subira mama,ipo siku utamjua the really
Samson".
Siku moja wakati Teresia anasafisha nyumba, akaamua atoe nguo zote
kabatini ili azikung'ute vumbi la kabati, alipotoa nguo za Samson, pakiti
iliyojaa unga kama wa ngano ikadondoka, Teresia akaichukua na kuichunguza kama
imetoboka au la, alipoona hakuna sehemu iliyotoboka, akaamua kuirudisha sehemu
alipo ikuta kisha akapanga nguo kama zilivokuwa. Samson aliporudi, Teresia
akamuuliza kuhusu ile paketi ya unga. Samson akahamaki,
"nani aliyekuambia uchakure nguo zangu?".
Teresia
akamwambia,
"sam, mbona umestuka hivo kama nimeua?, nilikuwa
napanga nguo vizuri kabatini na kwabahati mbaya hiyo pakiti ikaanguka, kama
nilifanya kosa kwa kupanga nguo zako vizuri, naomba
unisamehe na nakuahidi
sitogusa tena nguo zako zikiwa kabatini".
Samson akaona kuwa huo ndio muda muafaka wa kumueleza
Teresia kazi anayofanya. Teresia alipotulia, Samson akamwambia,
"hujafanya kosa kupanga nguo zangu, na pengine hii
itanipunguzia wahaka niliokuwa nao".
Teresia akashangaa maana hakuelewa Samson alichokuwa
anaongea,
"una maanisha nini unaposema nimekupunguzia
wahaka?".
"Tere my dear, si unajua nikiasi gani ninavo kupenda?".
"najua
Sam hata mimi nakupenda sana ila sijaelewa nini unachomaanisha".
Samson akamsogelea Teresia na kukaa, akashika viganja
vyake, akamuambia,
"kwanza nitakayo kueleza, usije ukamueleza mtu
yoyoteyule, yote yaishie humu ndani, sawa?".
"mbona wantisha Sam?, yote haya
yanahusiana na ile pakiti niliyoiona? au kuna jambo lingine".
"inahusiana na
hiyo pakiti, kwani unajua kuwa ni kitu gani
kilichopomle ndani ya pakiti?".
"sijui ila niliona imefanana kama unga
wa ngano vile".
"ule sio unga wa ngano,inaitwa COCAIN".Samson aliposema
hivo,akatulia ili kumpima Teresia kuwa amezichukuliaje hizo habari. Teresia
aliposikia neno COCAIN,midomo ikaanza kumcheza,asijue la
kusema,akabaki akiwa
ameachama mdomo kwa mshangao. Samson alipoona kuwa Teresia amestuka sana,
akamuambia, "Tere darling, mbona umestuka hivo?, ile sio sumu ni kilevi tu kama
vile pombe".
"sikutegemea kitu kama hicho,si unajua kuwa cocain ni
haramu?".
"niharamu kama unataka iwe haramu,nisikilize kwa makini
Tere,umekuwa unaniuliza mara kwa mara kuwa kazi nafanyia wapi na mara zote
nimekuwa nakuambia uvute subira".
"ndivo ila sioni kufanya kwako kazi
kunahusiana vipi na cocain".
Samson ameamua kumpa
siri ya kazi yake Teresia ? je Teresia ataweza kuficha siri hiyo?,nini chanzo
cha Samsoni kutoonekana,na amekimbilia wapi? je nini kitatokea akigundulika
alipo? usikose sehemu ya kumi ya hadithi
hii...itaendelea....